Loading...

Kuhusu Sisi

Fursa Foundation ipo kwa ajili ya kumsaidia kijana

Uhalisia wa maisha kwa sasa unahitaji umakini zaidi kwenye kufanya maamuzi zaidi ya ilivyokuwa awali, wazee wetu walitumika sana kuchukua nafasi ya washauri ( Consultants & Mentors ) , hii ilipelekea kutengeneza mzani sawia kati ya asili, heshima, maadili, kazi nakadhalika kwa sababu jamii iliangalia sana kupata maelekezo na uwezo kutoka kwa wazee wetu, lakini kwa sasa mambo yamebadilika muingiliano wa IMANI, TAMADUNI, UTANDAWAZI na TEKNOLOJIA.....Aina za ukuaji tunazojihusisha nazo moja kwa moja.

Kukua Kiuchumi

Kukua Kiakili

Kukua Kiimani

Kukua Kijamii

Kukua Kihisia

KUA

kwa hatua sahihi

HUDUMA ZETU

Fursa Foundation inatoa huduma zifuatazo.

Huduma ya Ushauri

Kupitia Fursa Foundation utaweza kupata huduma ya ushauri kwa masuala mbalimbali ikiwemo imani, maisha, biashara, uchumi na mahusiano. Haya ni maeneo ambayo vijana wengi wameshindwa kuvuka salama aidha kwa kukosa uangalizi sahihi ama maarifa sahihi ya kufikia malengo yao.

Soma Zaidi

Semina

Kupitia Fursa Foundation tunatoa pia semina mbalimbali kwa vijana,wazazi,familia, shule na makanisa kwa ujumla, semina kwa ajili ya kujitambua na maarifa kwa watu wote kwani changamoto ya maarifa sio ya pande moja ukimuelimisha baba na mtoto hana elimu tambua kutakuwa na mvutano hivyo kupitia Fursa Foundation utaweza kuwa na semina ya familia ambayo itaruhusu wanafamilia wote kujumuika na kupata elimu pamoja, lakini hata kwa ngazi nyingine lengo ni kukua kwa hatua sahihi.

Soma Zaidi

Mafunzo

Kupitia Fursa Foundation tunatoa semina kozi za mafunzo ya ufundi stadi ili kuongeza ujuzi na maarifa kwa watu, ufundi stadi ni mbadala mzuri wa kipato chako ukiwa na maarifa ya kufanya vitu vingi maana yake ni unakuwa na fursa nyingi zaidi, tunatoa mafunzo kulingana na ratiba na mpangilio wa kalenda ya mwaka hivyo endelea kuwa karibu na mitandao yetu ama acha namba za simu sehemu ya mawasiliano nasi tutakujulisha kwa wakati sahihi.

Soma Zaidi

Msaada

Fursa Foundation tunatoa msaada wa hali na muda mwingine mali, kulingana na uhitaji lakini pia uwezo wa huduma, matarajio yetu ni kutatua changamoto zilizoko ndani ya uwezo wetu kwa wale wanaotufikia kwa msaada zaidi ya ushauri na ushauri wa kitaalam zaidi.

Soma zaidi

FAQ's

Maswali ya ufahamu zaidi

Baadhi ya maswali na majibu kwa ufahamu zaidi wa Fursa Foundation na jinsi unavyoweza kunufaika na ushirika nasi.

Una swali zaidi

A: Hapana huduma kutoka Fursa Foundation sio kwa ajili ya vijana peke yao, japokuwa kundi kubwa linaloangaliwa ni vijana kwa kuwa ndio wanakutana na changamoto nyingi katika maamuzi na makuzi yao, lakini tunatoa huduma kuanzia kwa mtoto hadi mzazi

A: Ndio, moja ya K5 zetu za kukua ni Uchumi, na uchumi unahitaji sana biashara na uimara wake hivyo tunajihusisha moja kwa moja na uanzishaji,usajili,usimamizi na ukuzaji ikiwa sehemu ya kuhakikisha malengo na mafanikio yake.

A: Ndio, zipo gharama za kupokea huduma zetu kwa baadhi yake na pia zipo nyingine ambazo zinatolewa bure kabisa kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa uhitaji wako nasi tutakufahamisha zaidi.

A: Kujiunga na huduma zetu ni rahisi sana, fuata fomu yenye maswali kadhaa ya ufahamu na utambuzi kisha weka mawasiliano yako kisha sisi tutawasiliana na wewe ama unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia ukurasa wa mawasiliano.