FURSA FOUNDATION ni huduma ama fursa ya kijana kujifunza hatua kwa hatua makuzi sahihi katika nyanja ya KIIMANI,KIUCHUMI, KIJAMII, KIAKILI NA KIHISIA kupitia huduma ya
Kupitia Fursa Foundation utaweza kupata huduma ya ushauri kwa masuala mbalimbali ikiwemo imani, maisha, biashara, uchumi na mahusiano. Haya ni maeneo ambayo vijana wengi wameshindwa kuvuka salama aidha kwa kukosa uangalizi sahihi ama maarifa sahihi ya kufikia malengo yao.
Tunao washauri wakufunzi na wabobevu katika kila nyanja ambayo unahitaji msaada, msingi wa mafanikio ni ushauri bora na ukiwa unahitaji kufanikiwa kwenye maisha yako basi unahitaji kuwa na washauri sahihi kwenye safari yako ukiwa hapa duniani. Karibu leo tuzungumze changamoto yako sio mwisho wa tumaini na maarifa yako, kwetu tunasema mtazamo juu ya changamoto yako ni ushindi 50% kabla ya kutatua changamoto yako.
Zungumza nasi
Kupitia Fursa Foundation tunatoa pia semina mbalimbali kwa ngazi zote ikiwa ni watoto vijana,wazazi,familia, shule na makanisa kwa ujumla, semina kwa ajili ya kujitambua na maarifa ambayo yatakuwa ni chachu ya mafanikio na mlengo chanya.
Changamoto ya maarifa sio ya pande moja ukimuelimisha baba na mtoto hana elimu tambua kutakuwa na mvutano wa maarifa lakini pia ukimuelimisha mtoto bila mzazi hawezi kufikia malengo, na hapa kumekuwa na ombwe kubwa la mawasiliano kati ya wazazi na watoto, mawasiliano yamekuwa hafifu na sio yenye nguvu kulingana na mtindo wa maisha na majukumu.
Hivyo kupitia Fursa Foundation tunafanya semina kwa ngazi zote ikiwa ni familia hadi jumuia zipo semina ambazo tunaziandaa wenyewe lakini pia unaweza kuwasiliana nasi kwa ajili ya semina binafsi, nyumbani, ofisini, kanisani n.k nasi tutafika na kufanya kwa weledi na ubora wa hali ya juu lengo likiwa ni kufikia mafanikio lengwa.
Wasiliana nasi
Kupitia Fursa Foundation tunatoa semina kozi za mafunzo ya ufundi stadi ili kuongeza ujuzi na maarifa kwa watu, ufundi stadi ni mbadala mzuri wa kipato chako ukiwa na maarifa ya kufanya vitu vingi maana yake ni unakuwa na fursa nyingi zaidi
Zama tulizokuwa nazo wingi wa ujuzi unakupa nafasi zaidi ya kufanikiwa, tunatoa mafunzo kulingana na ratiba na mpangilio wa kalenda ya mwaka hivyo endelea kuwa karibu na mitandao yetu ama acha namba za simu sehemu ya mawasiliano nasi tutakujulisha kwa wakati sahihi.
Wasiliana nasi
Fursa Foundation tunaamini kuwa pamoja na kuwa na huduma hizo wapo wahitaji ambao wanahitaji msaada zaidi ya kujitambua na maarifa kulingana na uhitaji wao hivyo tukawiwa kuwa na huduma ya kutoa msaada ambao utakuwa zaidi kiwango chetu.
Matarajio yetu ni kutatua changamoto zilizoko ndani ya uwezo wetu kwa wale wanaotufikia kwa uhitaji wao, tunaamini katika kushikana mkono na mafaniko ya wengi ndio ukuaji halisi wa uchumi,Hivyo kwa kuzingatia hayo na kutambua malengo yetu unaweza kutuchangia kwa ajili ya kuwa na uwezo mzuri zaidi wa kushika watu wengi kadri tunavyoweza. Pia kwa mwenye uhitaji wa msaada tafadhali tuandikie kupitia njia zetu za mawasiliano ama bonyeza hapa chini kujaza fomu nasi tutawasiliana na wewe
Changia Msaada