Loading...

Miradi yetu

Fursa Foundation

Miradi tuliyonayo kwa sasa kwa ajili ya Maarifa na Kujitambua

KULEA MABINTI KWA UMRI

Fursa Foundation tunayo huduma ya kulea mabinti kwa kuwatofautisha umri ili kupokea malezi na maarifa tofauti na wengine yapo makundi 4 ambayo tumetofautisha

1. Miaka 10 - 17 ( Elimu ya kujitambua na kujiandaa/kutimiza na majukumu)

2. Miaka 18 - 24 ( Elimu ya kujitambua, kujisimamia na kusimamia malengo)

3. Miaka 25 - 30 ( Elimu ya utambuzi , uchumi na mafanikio)

Kupitia mradi huu tunategemea kutengeneza kizazi bora chenye kujitambua na maarifa sahihi ambayo yatamsaidia kijana kuwa na maamuzi ya maarifa na sio kufata mkumbo pamoja na mihemko.

Ili kujiunga jaza fomu hapa chini nasi tutawasiliana na wewe mara moja.

Zungumza nasi

MZAZI MJALI MWANAO

Fursa Foundation imeandaa program za kuwasaidia watoto kuanzia miezi 6 na kuendelea kwa ajili ya kuwasaidia kuepukana na madhara ya Teknolojia ikiwemo programu za simu,Tv na kadhalika changamoto kubwa inayotengenezwa na Teknolojia ni changamoto ya afya ya akili kwani vitu vingi vinatengenezwa kwa kujenga uraibu ( addiction) hivyo kupelekea kuathiri ukuaji, makuzi, afya na matendo pia, hili ni eneo jingine ambalo limewafelisha watu wengi hivyo kupitia program maalum za Fursa Foundation zitamsaidia mtoto wako kuepukana na changamoto ya afya ya akili lakini pia kwa yule ambae tayari amesha athirika namna asili ya kumboresha na kumrudisha vyema.

Wasiliana nasi