Loading...

Kuhusu Sisi

Stori Yetu

Fursa Foundation

Fursa Foundation - Kua kwa hatua sahihi.

Uhalisia wa maisha kwa sasa unahitaji umakini zaidi kwenye kufanya maamuzi zaidi ya ilivyokuwa awali, hapo awali wazee wetu walitumika sana kuchukua nafasi ya washauri ( Consultants & Mentors ) kwa vijana wa rika mbali mbali , hii ilipelekea kutengeneza mzani sawia kati ya asili, heshima, maadili, kazi nakadhalika kwa sababu jamii iliangalia sana kupata maelekezo na uwezo kutoka kwa wazee wetu.

Lakini kwa sasa mambo yamebadilika muingiliano wa IMANI, TAMADUNI, UTANDAWAZI na TEKNOLOJIA vimepunguza sana nafasi ya wazee kuwa muhimili wa jamii, kwa sasa jamii imegeukia imani, tamaduni,utandawazi na teknolojia kuwa msingi kwa kiasi kikubwa kupitia mafundisho ya imani,mtindo wa maisha ya tamaduni fulani, utu na maadili ya utandawazi pia mwongozo wa teknolojia. Vitu hivi vimeleta changamoto kwenye namna sahihi ya kuyaendesha maisha yetu huku kukiwa na asili ambazo tumezirithi kwenye damu ambazo hazihitaji muingiliano, hii imepelekea madhara kadha ambayo yamebadili na kuathiri kila nyanja ya makuzi bora.

Fursa General Enterprises Ni kampuni ya kizalendo iliyosajiliwa BRELA - 621358, chini ya chapa yake FURSA FOUNDATION tunakaona ipo haja ya kusaidia jamii kuweza kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinamlengo chanya hasa kwa watoto na vijana ambao ndio wako kwenye hatari kubwa ya uathiri wa makuzi, malezi na mazingira ( Mtindo wa maisha), ndipo tukakuanzishia chapa maalum kwa ajili ya kutatua changamoto hasi na kuzifanya ziwe chanya.

FAQ's

Maswali ya ufahamu zaidi

Baadhi ya maswali na majibu kwa ufahamu zaidi wa Fursa Foundation na jinsi unavyoweza kunufaika na ushirika nasi.

Una swali zaidi

A: Hapana huduma kutoka Fursa Foundation sio kwa ajili ya vijana peke yao, japokuwa kundi kubwa linaloangaliwa ni vijana kwa kuwa ndio wanakutana na changamoto nyingi katika maamuzi na makuzi yao, lakini tunatoa huduma kuanzia kwa mtoto hadi mzazi

A: Ndio, moja ya K5 zetu za kukua ni Uchumi, na uchumi unahitaji sana biashara na uimara wake hivyo tunajihusisha moja kwa moja na uanzishaji,usajili,usimamizi na ukuzaji ikiwa sehemu ya kuhakikisha malengo na mafanikio yake.

A: Ndio, zipo gharama za kupokea huduma zetu kwa baadhi yake na pia zipo nyingine ambazo zinatolewa bure kabisa kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa uhitaji wako nasi tutakufahamisha zaidi.

A: Kujiunga na huduma zetu ni rahisi sana, fuata fomu yenye maswali kadhaa ya ufahamu na utambuzi kisha weka mawasiliano yako kisha sisi tutawasiliana na wewe ama unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia ukurasa wa mawasiliano.